Ongea kwa Uhuru

Sema "hello" kwa tukio tofauti la ujumbe. Makini isiyotarajiwa ya faragha, pamoja na huduma zote unazotarajia.


"Ninatumia Signal kila siku."

Edward Snowden
Msema ukweli na bingwa wa faragha

"I trust Signal because it’s well built, but more importantly, because of how it’s built: open source, peer reviewed, and funded entirely by grants and donations. A refreshing model for how critical services should be built."

Jack Dorsey
CEO of Twitter and Square

"Signal ndicho chombo cha usimbaji fiche tulichonacho. Ni bure na hukaguliwa kirika. Ninawahimiza watu kuitumia kila siku."

Laura Poitras
Mtengenezaji wa filamu alieshinda tuzo ya Oscar na mwandishi wa habari

"Mimi huvutiwa mara kwa mara na wazo na utunzaji uliowekwa kwenye usalama na utumiaji wa programu hii. Ni chaguo langu la kwanza kwa mazungumzo yaliyosimbwa."

Bruce Schneier
Mtaalamu maarufu kimataifa wa usalama wa teknolojia

Kwanini utumie Signal?

Chunguza hapa chini kuona kwa nini Signal ni mjumbe rahisi, mwenye nguvu, na usalama

Shirikisha Bila Ukosefu wa Usalama

Usimbo fiche wa mwisho-hadi-mwisho (unaowekwa na Itifaki ya Signal ya chanzo huria) huweka mazungumzo yako salama. Hatuwezi kusoma jumbe zako au kusikiliza simu zako, na hakuna mtu mwingine anayeweza. Usiri sio njia ya hiari— ni njia tu ambayo Signal inafanya kazi. Kila ujumbe, kila simu, kila wakati.

Sema Chochote

Shirikisha kwa maandishi, ujumbe wa sauti, picha, video, Vihuishi Tuli na faili bure. Signal inatumia muunganisho wa data ya simu yako ili uweze kuepusha ada za Ujumbe Mfupi na Ujumbe wa Media.

Ongea kwa Uhuru

Piga simu wazi za sauti na video kwa watu ambao wanaishi katika jiji lote au kuvuka bahari, bila malipo ya umbali mrefu.

Fanya Faragha Ishike

Ongeza safu mpya ya kujieleza kwenye mazungumzo yako na vibandiko vilivyosimbwa. Unaweza pia kuunda na kushirikisha pakiti za vibandiko vyako.

Patana na Vikundi

Gumzo za vikundi hufanya iwe rahisi kuendelea kuungana na familia yako, marafiki, na wafanya kazi wenzako.

Hakuna matangazo. Hakuna wafuatiliaji. Hakuna mchezo.

Hakuna matangazo, hakuna wauzaji wa ushirika, na hakuna ufuatiliaji wa kuogofya kwenye Signal. Kwa hivyo zingatia kushirikisha nyakati unazojali na watu unaowajali.

Bure kwa Kila Mtu

Signal ni shirika huru lisilopata faida. Hatuhusishwi na kampuni yoyote kubwa ya teknolojia, na kamwe hatutanunuliwa na yoyote aidha. Maendeleo yanawezeshwa na ruzuku na michango kutoka kwa watu kama wewe.